STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 28, 2013

Megan Young ndiye Miss World, Tanzania kama kawa yaanguka

Miss World 2013, Megan Young.
Mshindi wa Pili Miss World 2013, Marine Lorphelin.
Mshindi wa Tatu 2013, Carranzar Naa Okailey Shooter.
KISURA toka Philippines, Megan Young ameibuka kidedea katika shindano la Miss World 2013 baada ya kunyakua taji hilo, huku Tanzania ikiendelea kuwa wasindikizaji.
Wakati mwakilishi wa Tanzania akishindwa kufurukuta, Mghana Carranzar Naa Okailey Shooter aliitoa kimasomaso Afrika bada ya kushika nafasi ya tatu miongoni mwa warembo 130 waliochuana katika shindano hilo.,
Megan amerithi taji hilo kutoka kwa mrembo wa China, Yu Wenxia aliyefanya hivyo mwaka jana.
Katika shindano hilo lililofanyika mjini Jakarta, Indonesia na kumalizika muda mfupi uliopita, mrembo kutoka Ufaransa, Marine Lorphelin alishika nafasi ya tatu.
Tanzania kama kawaida yake, haikuweza kabisa kufua dafu baada ya mshiriki wake, Brigitte Lyimo kushindwa kufurukuta katika mtanange huo mkali na unaobeba hisia kubwa miongoni mwa wadau wake duniani kote.
Dalili za Miss Ghana kung'ara katika shindano hilo zilizidi kuongezeka hasa kutokana na umahiri wake katika kujibu swali na kujiamini.

No comments:

Post a Comment