STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 28, 2013

David Moyes mambo magumu, Man United yanyukwa tena, City ikifa kwa Aston Villa EPL

http://i.huffpost.com/gen/1138374/thumbs/o-WAYNE-ROONEY-DAVID-MOYES-570.jpg?7
Wanafarijiana, Rooney na kocha wake, David Moyes

KOCHA David Moyes ameendelea kuwa na wakati mgumu kwenye Ligi Kuu ya England baada ya leo kulazwa mabao 2-1 nyumbani na timu ya West Bromwich Albion, huku majirani zao Manchester City wakigaragazwa ugenini kwa kipigio cha mabao 3-2 toka kwa Aston Villa.
Moyes aliyemrithi mikoba Sir Alex Ferguson koicha mwenye mafanikio makubwa kisoka katikka klabu hiyo na barani Ulaya, alijikuta vijana wake wakipokea kipigo cha pili mfululizo katika ligi hiyo baada ya wiki iliyopita kulala kwa Manchester City.
Wageni walitangulia kupata bao katika dakika ya 54 kupitia kwa Morgan Amalfitano kabla ya Wayne Rooney kusawazisha dakika chache baadaye na bao lililowakatisha tamaa Mashetani Wekundu lilitupiwa kambani na Saido Berahino dakika ya 67.
Nayo Manchester City baada ya kuwafunga mdomo mahasimu wao wa jiji la Manchester, leo haikuwa na chao mbele ya Astoni Villa kwa kulazwa mabao 3-2, huku Cardiff City wakipata ushindi ugenini dhidi ya Fulham na West Ham United ikilala bao 1-0 ugenini dhidi ya Hull City, na Southampton ikipata ushindi wa pili mfululizo kwa kuilaza Crystal Palace mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment