STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 30, 2013

Francis Miyeyusho 'amyeyusha' Momba kwa pointi

Bondia Sadiki Momba (kushoto) akionyeshana umwamba wa kutupiana makonde na Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika jana Jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es Salaam. Miyeyusho alishinda kwa pointi 
Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa  Friends Coner  Manzese Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa pointi 
Mwamuzi Sako Mtilya akimnyanyua mkono juu bondia  Francis Miyeyusho baada ya kumshinda kwa pointi mpinzani wake  Sadiki Momba wakati wa mpambano wao
Bondia Mussa Sunga kushoto akipambana na Fadhili  Awadh wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili. Awadh alishinda kwa Point 
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akitoa maelezo ya DVD zake zenye mabambano ya ngumi makali kwa ajili ya kuangalia na kujifunza ngumi nzito zenye msisimko zinazofanyika duniani kote kocha huyo wa mchezo wa masumbwi alikuwa akionesha DVD za Lenox Lewis, Manny Pacquaio,Muhammed Ali, Floyd Mayweather, na wengine kibao
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akitoa maelezo ya DVD zake zenye mabambano ya ngumi makali kwa ajili ya kuangalia na kujifunza ngumi nzito zenye msisimko zinazofanyika duniani kote kocha huyo wa mchezo wa masumbwi alikuwa akionesha DVD za Lenox Lewis, Manny Pacquaio,Muhammed Ali, Floyd Mayweather, na wengine kibao
Baadhi ya raia wa kigeni kutoka china waliokuja kumsapoti bondia Mussa Sunga wakiwa katika picha ya pamoja na bondia huyo
DVD KALI ZA MCHEZO WA NGUMI ZINAZOSAMBAZWA NA KOCHA SUPER D
Mashabiki wa mchezo wa masumbwi



BINGWA wa Kimataifa wa Ngumi za Kulipwa anayetambuliwa na IBO, Francis Miyeyusho ameendeleza rekodi yake ya kuwachakaza wapinzani wake baada ya mwishoni mwa wiki kumshinda kwa pointi Sadick Momba.
Miyeyusho alipata ushindi huo siku ya Jumapili katika pambano lisilo la ubingwa lililochezwa kwenye ukumbi wa Friends Corner, Manzese jijini Dar es Salaam.
Miyeyusho aliyemchakaza hivi karibuni Mzambia Fidelis Lupupa, alionyesha tangu mwanzoni mwa mchezo huo dhamira yake ya kuibuka ushindi, licha ya Momba kuonyesha upinzani mkubwa.
Wakiviziana na kudonoana kwa zamu, mabondia hao walijikuta wakimaliza pambano hilo la uzito wa bantam bila mashabiki kutabiri mapema nani mshindi kutokana na waliovyoonyesha upinzani katika mchezo huo.
Hata hivyo baada ya kumalizika kwa mchezo na majaji kutoa matokeo yao, mwamuzi Sako Mtilya alimtangaza Miyeyusho kuwa ndiye mshindi na kufanya mashabiki waliofurika kwenye ukumbi huo kumshangilia bondia huyo.
Huo ni ushindi wa 12 mfululizo kwa Miyeyusho ndani ya ardhi ya Tanzania tangu Aprili 2009 akiwapiga mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo katika kipindi hicho, bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 47 na kushinda 36 akipoteza 10 na kuambulia sare mbili alishatoka nje ya nchi mara tatu na mara zote kudundwa na wapinzani wake kwa KO.
Katika pambano jingine la utangulizi Fadhili Awadh alimshinda kwa pointi Mussa Sunga katiika pambano lililokuwa limekaa ufundi.

No comments:

Post a Comment