STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 11, 2013

Lampard aiweka pazuri Chelsea EPL

Frank Lampard: Chelsea's history man.
Frank Lampard akishangili moja ya mabao yake yanayomfanya azidi kuimarisha rekodi yake ya mabao 'Darajani'

MAGOLI mawili kupitia kwa kiungo mzoefu, Frank Lampard yameiweka pazuri Chelsea katika kujihakikishia kuwepo kwenye Top $ ya kushiriki  moja kwa moja Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya jioni hii kuitambia Aston Villa nyumbani kwa mabao 2-1.
Chelsea kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya dakika ya 61 na 88 ya kiungo huyo mkongwe ambaye kadri siku zikizidi kuyoyoma anazidi kuonyesha umuhimu wake 'Darajani' yameifanya waliokuwa mabingwa hao wa Ulaya kufikisha pointi 72, akisaliwa na mechi moja.
Arsenal ambayo itashuka dimbani Jumanne kupepetana na 'vibonde' Wigan Athletic ndiyo pekee inayoweza kuzivuka pointi ilizonazo Chelsea na kuweza kuitoa kwenye tatu bora, lakini uhakika wa 4 Bora imeshaupata kwa ushindi huo wa leo.
Katika pambano la leo Chalsea walishtuliwa na bao la robo ya kwanza ya kipindi cha kwanza kupitia Christian Benteke bao lilodumu hadi mapumziko ambapo wageni walijikuta wakimaliza pungufu baada ya Ramires kupewa kadi ya pili ya njano na kusindikizwa na nyekundu na mwamuzi Lee Stephen Mason.Hata hivyo wenyeji nao walijikuta wakimpoteza mchezaji wao muhimu Benteke kwa kulimwa kadi ya pili ya njano kama ilivyokuwa kwa Ramires na kutolewa nje kwa kadi nyekundu na kutoa mwanya kwa wageni kufunga bao la kusawazisha kabla ya kuwazima dakika za lala salama na kuwaacha na pointi zao 40 wakiendelea kupumua katika janga na kushuka daraja kama haitashinda mechi ya mwisho na waliopo nyuma yake kushinda michezo yao kesho na siku ya Mei 19.
Mabao hayo mawili yamemfanya Lampard kufikisha jumla ya mabao 203 mpaka sasa katika michuano yote kati ya mechi 606.

No comments:

Post a Comment