STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 5, 2013

Fernando Torres yainusisha Chelsea Nusu Fainali, Newcastle yafa ugenini

Torres akifunga moja ya mabao yake jana usiku

WAKATI mabao mawili ya nyota wa Hispania, Fernando Torres jana yakiiwezesha Chelsea kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Rubin Kazan ya Russia, 'ndugu' zao, Tottenham Hotspurs ilijikuta iking'ang'aniwa nyumbani na Basel katika mechi za Robo Fainali ya UEFA Ndogo ya Ulaya.
Torres maarufu kaa El Nino alifunga bao la kwanza dakika ya 16 na jingine dakika ya 70, huku bao jingine likitumbukizwa kimiani na Victor Moses na kufanya Chelsea kujitengenezea nafasi nzuri ya kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo.
Mpaka mapumziko mabao yalikuwa 2-1, Kazan wakipata bao pekee katika kipindi cha kwanza baada ya kutanguliwa kufungwa mabao mawili na Chelsea kupitia kwa Bibras Natcho kwa penati.
Katika mechi nyingine iliyochezwa London ya Kaskazini, Tottenham ikiwa nyumbani ilibanwa na Basel na kuambulia sare ambapo hadi mapumziko tayari walishaumizwa mabao 2-1.
Valentin Stocker alifunga bao la kuongoza kabla ya dakika nne Fabian Frei kuongeza la pili na Emmanuel Adebayor kurudisha moja dakika chache kabla ya mapumziko.
Mchezaji Gylfi Sigurdsson aliyeingia kuchukua nafasi ya Aaron Lennon aliyeumia aliiokoa Tottenham baada ya kufunga bao la kusawazisha kwenye dakika ya 58 na kuipa kazi kubwa vijana hao wa AVB kujipanga kwa mechi ya marudiano wiki mbili zijazo huko Russia.
Nao vijana wa Newcastle United wakiwa ugenini nchini Ureno ilikumbana na kipigo cha mabao 3-1 mbele ya wenyeji wao Benfica na kutoa nafasi ndogo kwa vijana hao wa Uingereza kupenya hatua inayofuata ya michuano hiyo.
Papiss Demba Cisse alitangulia kuifungia Newcastle bao katika dakika ya 13 kabla ya Rodrigo kusawazisha bao hilo dakika 25 na kufanya matokeo hadi wakati wa mapumziko kuwa 1-1.
Kipindi cha pili wenyeji walicharuka kwa kupata mabao yake mawili ndani ya dakika sita tu, Lima akifunga la pili dakika ya 65 kabla ya Cardozo kuongeza la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 71.
Katika pambanbo jingine lililochezwa jana katika michuano hiyo, Fenerbache ya Uturuki ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wageni wao Lazio.
Pierre Webo aliifungia wenyeji bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kabla ya nyota wa zamani wa Livrpool Dirk Kuyt na kuwafanya Fenerbenche kujiweka mguu sawa kutunga nusu fainali iwapo iutaenda kukomaa ugenini wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment