STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 24, 2013

Washukiwa 10 wakamatwa tukio la Westgate Kenya

jengo lililokuwa likionekana kwa mbali likifoka moshi
WAKATI jeshi la Kenya likikaribia kumaliza udhia katika tukio la kigaidi lililotokea jengo la Westgate, Nairobi inaelezwa watu 10 wametiwa mbaroni wakihusishwa na tukio hilo lililosababisha vifo vya watu karibu 70 na wengine 180 walio majeruhi.
Kwa mujibu wa matangazo ya BBC yaliyomkunuu Waziri wa Mambo ya Usalama wa Kenya, Joseph Ole Lenku, alisema watu hao walikamatwa kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya Jomo Kenyatta na maeneo mengine baada ya kushukiwa siyo watu wazuri.
Hata hivyo waziri Lenku alisema kukamatwa kwa watu hao hakuna maana kwamba ndiyo wamemaliza operesheni au ni watuhumiwa halisi wa tukio hilo, isipokuwa wanaendelea kufanya uchunguzi kwa kina ili kubainia kama wanahusika au la kisha kujua hatua za kuwachukulia.
Kuhusu operesheni inayoendelea katika tukio hilo lililotokea juzi, waziri alisema jeshi na vikosi vya polisi vimefanikiwa kuthibiti jengo hilo na kusema muda wowote watakamilisha kazi kwa kuwatia mikononi waliohusika na tukio hilo ambapo mpaka sasa watekaji wawili wanadaiwa kuuwawa.
Waziri huyo alidokeza kuwa watekaji hao wanaodaiwa ni kikosi cha Al Shabaab walijaribu kujinusuru kwa kuchoma sehemu ya jengo na kusababisha kuonekana kwa moshi mkubwa angani mchana wa jana, lakini jeshi lilifanikiwa kulikamata jengo hilo kwa asilimia kubwa.

No comments:

Post a Comment