Chelsea wakishangilia bao lao lililofungwa na Fernanndo Torres |
Atletico wakipambana kuwania kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya |
Chelsea ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Stanford Bridge ilishindwa kuhimili makali ya wapinzani wao na kukubali kuondolewa kwa mara ya kwanza na timu za Hispania katika hatua hiyo baada ya kutandikwa huku wakishuhudiwa na gwiji wa zamani wa Argentina, Diego Maradona.
Vijana wa Mourinho walitangulia kupata bao la kuongoza lililofugwa na nyota wa zamani wa Atletico, Fernando Torres katika dakika ya 36 kabla ya wageni kusawazisha kupitia kwa Adrian dakika moja kabla ya kwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilikuwa kibaya kwa Chelsea baada ya Atletico kupata bao la pili lililofungwa kwa penati na Diego Costa katika dakika ya 60 kabla ya Tuiran kuongeza bao la tatu dakika ya 72 na kuihakikishia Atletico kutinga fainali za michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20 iliyopita.
Timu hiyo sasa itakutana na mahasimu wao, Real Madrid iliyowavua taji Bayern Munich juzi kwa kuicharaza mabao 4-0 nyumbani kwao na kufuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 5-0 baada ya mechi ya kwanza mjini Madrid kupata ushindi wa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment