MSHAMBULIAJI nyota wa
klabu ya Liverpool Luis Suarez amezidi kuongeza tuzo katika kabati lake la kuhifadhia tuzo
zake, baada ya kuteuliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Uingereza
msimu wa 2013-2014.
Nyota huyo aliyefunga mabao 31 na kutoa pasi 12 za
mabao katika mechi 33 za ligi alizocheza, huku timu yake Liverpool
ikizidiwa kidogo na Manchester City katika mbio za ubingwa, poia ndiye mfungaji bora wa ligi hiyo.
Suarez,
ambaye pia ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji wa PFA na
Mchezaji Bora wa Waandishi wa habari za Soka msimu huu, ameshinda tuzo
ya nne msimu huu pamoja na ile ya kiatu cha dhahabu.
Tuzo hiyo Suarez
imekuja ikiwa ni saa chache baada ya meneja wa Liverpool Brandan Rodgers
naye kutunukiwa tuzo ya kocha bora wa mwaka na Chama cha Makocha wa
Ligi nchini humo.
Rodgers amekuwa na msimu mzuri akiiongoza timu hiyo ya
Merseyside kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi.
Kocha wa timu ya taifa
ya Uingereza, Roy Hodgson ndiye alimkabidhi tuzo hiyo kocha huyo mwenye
umri wa miaka 41, ambayo hutokana na kura zinazopigwa na makocha kutoka
timu za madaraja yote manne.
Kabla ya hapo mshambuliaji huyo alikuwa na wakati mgumu kutokana na matukio ya utovu wa nidhamu yaliyomsababisha kufungiwa kucheza mechi kadhaa na kutoza faini kwa kumbagua Patrick Evra na kung'ata beki wa Chelsea.
No comments:
Post a Comment