STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 3, 2014

Nyota Mtibwa, JKT waibeba Mbogamboga 'mchangani'

Mtibwa Sugar

Na Adam FungamwangoWACHEZAJI wa Mtibwa Sugar Mohamed Mkopi, Mohamed Ally 'Gaucho' na Jamali Machelenga wa JKT Ruvu, juzi waliibeba timu ya Mbogamboga FC ya Mwananyamala kuifunga Rendts ya Mikocheni mabao 3-2 kwenye uwanja wa shule ya msingi Mwananyamala.
Baada ya Ligi Kuu kumalizika wachezaji wa timu za Ligi Kuu wameshaanza kujimwaga kwenye viwanja vya mchangani wakizichezea timu zao za mitaani au kukodishwa kwa madau makubwa kwenye michuano mbalimbali nchini, hususan jijini Dar es Salaam.
Mastaa hao waliichezea timu hiyo kwenye michuano mipya iliyoanzishwa ya Wadau Cup iliyopanza wiki iliyopita kwenye uwanja huo na kuzishirikisha jumla ya timu 16 kutoka wilaya zote tatu katika jiji la Dar es salaam.
Michuano hiyo imeanzishwa na baadhi ya viongozi wa chama cha soka Kinondoni (KIFA) Gomigo Mketo na mratibu wake Omari Firigisi.
Uzoefu wa wachezaji hao wa Ligi Kuu ndiyo kwa kiasi kikubwa ulioibeba Mbogamboga kwani walikuwa wakipelekeshwa na vijana wasio na majina makubwa wa Rendts.
Mshambuliaji huyo wa Mtibwa alifunga goli la kwanza katika dakika ya tatu na kutengeneza bao la tatu baada ya kuachia shuti kali lililotemwa na kipa, kabla ya kumkuta mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar Laurent Mugia na kuuweka wavuni.
Bao lingine la washndi lilifungwa na Kibwana Kibwana, huku mawili ya Rendts yalifungwa na Daudi Iddi na Dicky Daudi.

mwisho

No comments:

Post a Comment