MSHAMBULIAJI nyota wa AC Milan na timu ya taifa ya Italia, Mario Balotelli anakabiliwa na changamoto ya kuwa fiti kabla ya mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia kutokana na kusumbuliwa na majeraha madogo ya msuli.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kuwa mchezaji muhimu katika mpango ya kocha Cesar Prandelli kwa ajili ya michuano hiyo baadae mwezi huu haswa kutokana na kuenguliwa kwa Giuseppe Rossi katika kikosi hicho.
Mkongwe Antonio Cassano na washambuliaji Alessio Cerci, Ciro Immobile na Lorenzo Insigne ndio wanatarajiwa kuwa mbadala katika safu ya ushambuliaji kama Balotelli hatakuwa fiti kwa asilimia mia moja. Kocha wa Italia Enrico Castlellaci amebainisha kuwa nyota huyo wa zamani wa Manchester City alipata majeraha ya msuli wakati akiwa kambini na timu hiyo huko Coverciano hivyo kumaanisha anaweza kukosa mechi ya ufunguzi dhidi ya Uingereza itakayochezwa huko Manaus Juni 14 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment