STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 12, 2015

TIMU ya Taifa ya Beach Soccer kuwafuata Wakenya kesho

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni (beach soccer) inatarajia kurusha karata yake ya kwanza Jumapili kwa kucheza na Kenya katika raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa ajili ya fainali za Afrika za michuano hiyo zitakazofanyika Aprili mwaka huu nchini Shelisheli.
Mchezo huo utachezwa Mombasa nchini Kenya na mchezo wa marudiano utachezwa nchini kati ya Februari 20 na 22 mwaka huu
Akizungumza jijini, Kocha wa timu hiyo John Mwansasu, alisema maandalizi ya kwa ajili ya mchezo huo yanaendelea vema na wamecheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Zanzibar na kusema walipoteza mmoja na kushinda mmoja.
 “Maandalizi yanaendelea na kiwango cha wachezaji kinaimarika kila siku na nawaahidi watanzania kurudi na ushindi japo sikupata michezo ya kirafiki ya kimataifa lakini nina imani na timu yangu”, alisema Mwansasu.
Kocha John Mwansasu anasaidiwa na Ali Shariff 'Adolf' kutoka Zanzibar, na Meneja wa timu ni George Lucas na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa ufukweni (beach soccer) kinaundwa na wachezaji  15, saba toka Zanzibar na nane Tanzania bara
Iwapo timu ya Tanzania itasonga mbele, katika raundi ya pili itacheza na Misri ikianzia nyumbani kati ya Machi 13 na 15 mwaka huu.
Timu hiyo inayofanya mazoezi kwenye ufukwe wa Escape One inatarajiwa kuondoka nchini kesho Ijumaa.

No comments:

Post a Comment