STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 5, 2013

BFT yafurahia mafanikio ngumi za taifa

KATIBU Mkuu wa BFT Makore Mashanga

UONGOZI wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limesema limefurahishwa na mafanikio iliyopatikana katika michuano ya klabu bingwa ya mchezo huo nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Michuano hiyo iliyoanza rasmi Januari 27 na kumalizika Februari 2 kwenye uwanja wa Ndani wa Taifa, kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga ilifanyika kwa ufanisi mkubwa tofauti na michuano iliyopita.
Katibu huyo alisema tangu ilipoanza mpaka ilipomalizika michuano yao ilifana na kushuhudia vipaji vipya toka klabu zilizoshiriki ambao alidai baadhi yao huenda wakaongezwa kwenye timu ya taifa ya mchezo huo.
"Tunashukuru michuano ya mwaka huu imekuwa na ufanisi mkubwa kukiwa hakuna malalamiko ya aina yoyote kama miaka miliyopita, huku vipaji vipya katika ngumi vikiibuka na kutuma matumaini," alisema Mashaga.
Mashaga alisema katika michuano hiyo kulikuwa na jopo la wajumbe wa kamati ya utendaji ambao ilikuwa ikifuatilia wachezaji kwa ajili ya kuteua wachezaji wa kujiunga timu ya taifa kwa michuano ijayo ya kimataifa.
Katika hatua nyingine, Mashaga alisema kozi ya ukocha wa awali ya ngumi imeanza jana chini ya mkufunzi mkuu, Meja Mstaafu Michael Changarawe.
Zaidi ya washiriki 20 wanatarajia kuchukua mafunzo hayo ya ngumi ya muda wa wiki moja ambapo wahitimu watatunukiwa vyeti sambamba na kutambuliwa rasmi na kupata kibali cha kufundisha kokote ngumi nchini.

Mwisho

No comments:

Post a Comment