STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 27, 2013

Coastal yashindwa kuiengua Simba 3 Bora

Kikosi cha Coastal Union


MABINGWA wa zamani wa Tanzania, Coastal Union leo wameshindwa kuiengua Simba kwenye nafasi ya tatu katika msim amo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Ruvu Shooting.
Coastal iliyokuwa kwenye dimba la nyumbani la Mkwakwani Tanga, ilikuwa na nafasi ya kuishusha nafasi ya tatu Simba ambayo haikushuka dimbani leo kwa vile inajiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya watakaokuwa wenyeji wao Libolo Fc ya Angola iwapo ingeilaza Ruvu.
Suluhu hiyo imeifanya wagosi hao wa Kaya kufikisha pointi 31 sawa na Simba na kuendelea kusalia kwenye nafssi yake ya nne kwa kuzidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Taarifa kutoka Tanga zinasema kuwa mchezo huo wa leo ulikuwa mkali na wenye upinzani mkali na ilionekana kama Coastal wangeweza kuibuka na ushindi kama sio uimara wa kikosi cha vijana wa Charles Boniface Mkwasa.












































































































































































































































































































No comments:

Post a Comment