STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 10, 2013

Simba yawatafuta Wagosi wa Kaya Taifa


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo imezinduka kwa kuweza kuilaza Coastal Union ya Tanga mabao 2-1 katika mechi yao ya kwanza ikiwa chini ya kamati maalum ya ushindi inayoongozwa na Malkia wa Nyuki.
Ikichezesha asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi cha pili, Simba ilionyesha uhai licha ya kusubiri mpaka dakika za lala salama za kipindi cha kwanza kuweza kupata mabao yake ya chapchap na kwenda mapumziko wakiongoza 2-0.
Mrisho Ngassa aliiandikia Simba bao dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza na dakika moja baadae Haruna Chanongo aliiongezea Simba timu yake bao la pili akimalizia pasi ya Ngassa na kufumua shuti lililomshinda kipa Shaaban Kado.
Kipindi cha pili, Coastal waliokuwa wamelipania pambano hilo ili wakalie nafasi ya tatu, walionyesha uhai na kufanikiwa kupoata bao lao la kufutia machozi lililofungwa katyika dakika ya 50 lililofungwa na kiungo Razak Khalfan bao lililofanya hadi mwisho wa mchezo matokeo kusomeka hivyo kwa Simba kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1.
Kwa matokeo hayto Simba imeendelea kukalia nafasi ya tatu ikifikisha pointi 34 tatu nyuma ya Azam wote wakiwa wamecheza mechi 19 sawa na vinara Yanga wanaoongoza kwa pointi 45.
Katika pambano la leo Simba ilipangwa hivi; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Hassan Hatibu, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Rashid Ismail/Salim Kinje, Abdallah Seseme, Haruna Chanongo na Mrisho Ngassa/Ramadhan Singano ‘Messi’.
Coastal Union; Shaaban Kado, Hamad Hamisi, Abdi Banda, Mbwana Hamisi, Philip Mugenzi, Razak Khalfan, Daniel Lyanga/Twaha Shekuwe, Mohamed Athumani, Deangelis da Silva, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Joseph Mahundi/Castory Mumbara. 

No comments:

Post a Comment