STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 4, 2013

Ajali yapoteza uhai wa watu 7 papo hapo, 44 wakimbizwa hospitalini

BASI la Taqwa linalofanya safari zake kati ya Tanzania na Zimbabwe, limepata ajali na kusababisha vifo vya watu saba huku wengine 44 wakijeruhiwa.
Habari zilizopatika hivi karibuni zinasema kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo la kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi mkoani Mufindi wakati basi hilo likitokea Dar kuelekea Zimbabwe.
Inaelezwa ajali hiyo ilihusisha magari matatu ambayo ni basi la Taqwa aina ya Nissan Diesel lenye namba za usajili T 273 CBR (Sniper), lori la mizigo aina ya Scania, mali ya Kampuni ya Nyati Transport Ltd lililokuwa limebeba shehena ya viazi pamoja na lori la mizigo lenye namba T 104 BZZ aina ya Scania, mali ya kampuni ya Sogea Satom.
majeruhi wa ajali hiyo inaelezwa wamekimbizwa hpsitalini kwa matitabu, ambapo Dk Bakuza wa hospitali ya Mufindi aliwataja watu waliofariki katika ajali hiyo na miili yao kuhifadhiwa hapo ni; Abrahaman Abduli (32) ambaye ni dereva wa basi la Taqwa, Nassoro Rashid (27) ambaye ni kondakta wa basi hilo, Omari Muhusin, Alli Mussa, Joseph Charles, Emmi Kafute na maiti moja haijafahamika jina lake.
MICHARAZO inawapa pole waliofikwa na msiba huo na pia kuwaombea tahfif majeruhi wote waweze kupona, kadhalika tukiwataka walioguswa na mkasa huu kuwa na moyo wa uvumilivu na subira kwa kukumbuka kuwa Kazi ya MUNGU haina makosa.
MUNGU aziweke roho za marehemu mahali Pema Ameen

No comments:

Post a Comment