STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 4, 2013

Hull City yarejea Ligi Kuu England



KLABU ya Hull City imefanikiwa kuungana na Cardiff City kupanda Ligi Kuu ya England msimu ujao baada ya jioni hii kutoshana nguvu katika pambano la kufungia msimu wa Ligi Daraja la Kwanza England.
Hull City ikiwa kwenye dimba lake la nyumbani, Kingston Communications  vijana hao wa kocha Steve Bruce walifungana mabao 2-2 na Cardiff City iliyokuja kusawazisha bao dakika za lala salama kwa mkwaju wa penati.
Sare hiyo imeifanya Hull City kufikisha jumla ya pointi 79 na kung'ang'ania nafasi ya pili nyuma ya Cardiff iliyokuw ameshatawaza mabingwa wa ligi hiyo wiki iliyopita ilimaliza msimu ikiwa na pointi 83.
Timu hizo mbili zimeziachia timu za Watford, Leichester City, Crystal Palace na Brighton & Have Albion kuchuana zenyewe kuwania nafasi moja ya kuungana nao kwenye Ligi Kuu ya England msimu ujao.
Watford imemaliza ligi leo kwa kichapo, lakini ikisalia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 77 ambapo kama ingeshinda ingeweza kuipiku Hull City, Brighton wamekamata nafasi ya nne klwa kufikisha pointi 75 baada ya leo kuibuka na ushindi, kisha kufuatiwa na Crystal Palace iliyokusanya pointi 72 baada ya jioni hii pia kupata ushindi kama ilivyokuwa kwa Leichester City iliyoshinda na kushika nafasi ya sita kwa pointi zake 68 sawa na timu ya Bolton Wanderers iliyolazimisha sare na kushuka nafasi nafasi ya sita kwa tofauti na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Tayari timu mbili zilizoshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya England zimeshafahamika ambazo ni Reading na Queen Park Rangers, huku timu ya mwisho ikiwa inasubiriwa wakati ligi hiyo ikielekea kufikia ukingoni.

No comments:

Post a Comment