STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 6, 2013

Kalapina halingani na zogo la mtaa

Kalapina katika pozi

MSANII nyota wa miondoko ya Hip Hop nchini, Karama Masoud 'Kalapina' ameachia nyimbo mbili mpya ambazo alitarajiwa kuzitambulisha rasmi jana kwa mashabiki wake katika tamasha lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MICHARAZO juzi, Kalapina anayeliongoza kundi la Kikosi cha Mizinga, alisema nyimbo mpya ni 'Zogo la Mtaa' na 'Hawalingani na Sisi', alizorekodia katika studio za Kikosi Records.
Kalapina alisema wimbo wa 'Zogo la Mtaa' ameuimba kwa kushirikiana na Suma Labu na Gwalu wakati ule wa 'Hawalingani na Sisi' ameimba kwa kushirikisha wasanii walioibuliwa na kukuzwa na familia ya Kikosi yenye  maskani yake maeneo ya Kinondoni kama Sam Flezy, Zimwi na Abuu Gaidi.
Mkali huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kadhaa kama 'Harakati', 'Kufa na Kupona', 'Lawama', 'Maisha Yangu Muziki Tosha' na nyingine, alisema nyimbo hizo ni salamu kwa mashabiki wake kwa mwaka 2013 akiwa amepania kuwapa burudani zaidi pamoja na uhamasishaji katika harakati za kujikomboa.
Kalapina pia alisisitiza juu ya mipango yake ya kutaka kuwania kiti cha ubunge Jimbo la Kinondoni ambalo kwa sasa linashikiliwa na Idd Azan wa CCM.
Katika uchaguzi uliopita msanii na mwanaharakati huyo aliwania kiti cha udiwani Kata ya Kinondoni kupitia Chama cha CUF na kushindwa kwa kura chache na mpinzani wake kupitia CCM

No comments:

Post a Comment