STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, May 9, 2013

Katavi, Nyamagana, Mbeya yapata visura wake

SAFARI ya kuelekea kumpata mlimbwende wa taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 inazidi kushika kasi, pale vitongoji mbalimbali vitakaposaka washindi wao wikiendi hii.
Redd’s Miss Katavi, Redd’s Miss Nyamagana na Redd’s Miss Mbeya Municipal wanatarajiwa kupata washindi wao katika mashindano hayo.
Mratibu wa Redd’s Miss Katavi, Shadya Ameir alisema kila kitu kimekamilika na warembo 12 wanatarajiwa kupanda stejini katika ukumbi wa Katavi Resort ili kumpata mshindi keshokutwa Jumamosi.
Alisema katika shindano hilo kutakuwa na burudani za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu nchini, hivyo aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.
“Hiyo Jumamosi mambo yatakuwa makubwa zaidi, kwa sasa kila kitu kimekamilika, watu waje kwa wingi kushuhudia kile kitakachoendelea,” alisema.
Naye mratibu wa Redd’s Miss Nyamagana, Muhsin Mambo alisema shindano hilo litafanyika Jumamosi.
Alisema warembo 18 watapanda jukwaani huku burudani ikitolewa na msanii Recho, Lady Zena na mshereheshaji atakuwa Zembwela.
Aidha wakati vitongoji hivyo vikitarajiwa kufanya mashindano yao, tayari warembo wako kambini katika vitongoji mbalimbali kote nchini wakijiandaa kwa mashindano yao.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment