STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 7, 2013

Mkwasa aiponda Simba kwa Yanga Mei 18

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyhILGXEPzcg08Ou6VWhyphenhyphenGQ_bEGVRsjHkUwM-95WMFyKgoa3AmSEp0pQFl7LDHsP8AUvz0B1SdcA1_DqHCjiLzsmNFvGJVgE7hf4UYU6HgdkrfVXUq4_nOTvCDcVKeGrucIGKzxSSwSOHl/s1600/Charles-Boniface-Mkwasa1.jpg
Kocha Charles Boniface Mkwasa
Baadhi ya wachezaji 'yosso'wa Simba

KOCHA mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa, amesema kikosi cha sasa cha Simba kilichosheheni wachezaji chipukizi ni dhaifu mno dimbani na ni ndoto kuweza kuibuka na ushindi dhidi ya mahasimu wao Yanga, Mei 18.

Mkwasa nyota wa zamani Yanga na Taifa Stars, aliyasema hayo juzi baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, iliyoisha kwa vijana wake kulala mabao 3-1, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alisema licha ya ukweli kuwa kiwango cha mchezo hubadilika kutoka mechi moja hadi nyingine, lakini alichokishuhudia kwa Simba katika siku za karibuni, hakimpi matumaini ya ubora wa kikosi hicho kuweza kuifunga Yanga.

“Kwa kiwango cha Simba cha leo na siku za karibuni, nikiri wazi kwamba kuifunga Yanga ni ngumu, japokuwa katika soka hakuna lisilowezekana ndani ya dakika 90,” alisema Mkwasa ambaye pia aliwahi kuinoa timu hiyo na Twiga Stars.

Aidha, Mkwasa alisema katika mchezo wao wa juzi, anamtupia lawama Mwamuzi Athuman Lazi kwa madai aliwatoa mchezoni vijana wake na kuonekana kuibeba Simba katika maamuzi yake.

Naye Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, aliwapongeza vijana wake hususan chipukizi kwa jinsi ambavyo walijituma hadi kuibuka na ushindi huo na kudai kuwa ataendelea kuwatumia nyota hao endapo atafanikiwa kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Simba kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwa point 42, nyuma ya Azam FC pointi 47 na mabingwa Yanga pointi 57.
Chanzo:Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment