STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 26, 2013

Ommy Lax aachia mpya akisaka meneja

Ommy Lax katika pozi
MKALI wa wimbo wa 'Kioo Changu' alioimba na Matonya, Imani Omary 'Ommy Lax' ameachia wimbo mwingine mpya uitwao 'Wapotezee' huku akisaka meneja wa kuzisimamia kazi zake.
Akizungumza na MICHARAZO, Ommy Lax, alisema angependa kufanya kazi chini ya meneja ili kumuongoza katika majukumu yake baada ya mtu aliyekuwa akimtegemea ambaye ni mjomba wake, MP kuwa na majukumu mengine mazito binafsi.
"Natamani na ninasaka meneja wa kunisimamia kazi zangu, hivyo yeyote atakayekuwa tayari anaweza kuwasiliana nami tukae chini na kukubaliana, " alisema Ommy Lax.
Juu ya wimbo wake mpya, Ommy lax alisema ameimba na  mkali kutoka Watanashati, PNC na tayari umeanza kurushwa hewani.
Ommy Lax, alisema kazi hiyo mpya aliyorekodia kwa maprodyuza R Pino na The Timing, ni moja ya nyimbo kali kwa mwaka 2013.
Msanii huyo aliyejishughulisha na sanaa tangu akiwa shuleni na kutoa kazi ya kwanza mwaka 2006, alisema kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kutoa  video ya wimbo huo.
"Kaka nimepakua wimbo mpya uitwao 'Wapotezee' nilioimba na PNC, ni moja ya kazi bomba siyo mchezo mashabiki wasubiri kuisikia hewani na sasa nafanya mipango ya video yake, lakini muhimu naomba mtu ajitokeze anipige tafu kama meneja," alisema.

No comments:

Post a Comment