STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 19, 2013

Warembo Miss Tabata 2013 kutembelea Mbuga ya Mikumi

Miss Tabata wakiwa kwenye pozi ya picha ya pamoja



WAREMBO watakaoshiriki kinyang'anyiro cha shindano la Miss Tabata 2013 watatembelea mbuga ya  wanyama ya Mikumi wikiendi ijayo.

Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga mapema leo kuwa, lengo la ziara hiyo ni kukuza utalii wa ndani. Alisema kuwa warembo hao pia watapata fursa ya kujua vivutio vilivyomo kwenye mbuga hiyo iliyoko mkoani Morogoro.

“Hii siyo mara yetu ya kwanza kuwapeleka warembo wetu mbugani. Tumekuwa tukifanya kila mwaka,” alisema Kalinga.

Kapinga alisema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na CXC Africa.



Shindano la kumsaka Miss Tabata  litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

Wadhamini wa shindano hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.

Warembo watakaoshiriki kwenye shindano hilo linaloandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19),  Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19),  Rehema Kihinja (20),  Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na  Suzan Daniel (18).



Warembo watano watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.

Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.

No comments:

Post a Comment