STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 23, 2013

Kiemba, Sure Boy ndiyo Wanasoka Bora Tanzania 2012

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah akimpa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi, Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam

KIUNGO nyota wa timu ya Simba na Taifa Stars, Amri Kiemba amefanikiwa kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Tanzania iliyotolewa na Chama cha Wanasoka Tanzania, SPUTANZA, katika hafla iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam.
Kiemba amenyakua tuzo hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya Pepsi kwa ufanisi wake kwa msimu uliopita ambapo amekuwa katika kiwango cha juu akiisaidia kuifungia simba mabao 8 kwa msimu uliopita huku akiibeba Stars katika mechi zake za kimataifa.
Naye kiungo mwenye mapavu ya mbwa, Abubakar Salum 'Sure Boy' alinyakuwa tuzo ya Mwanasoka Bora Chipukizi, tuzo ambayo alistahili kutokana na umahiri wa mchezaji huyo anayeichezea Azam na Taifa Stars.
Wengine walionyakua tuzo katika hafla hiyo ni kipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif 'Casillas' aliyekuwa Kipa Bora wa Mwaka na kocha Mecky Mexime wa Mtibwa.
MICHARAZO inawapa pongezi wote waliotwaa tuzo hizo na kuwatakia mafanikio mema, kadhalika inawapa heko SPUTANZA na wadhamini wa tuzo hiyo ya kwanza kuandaliwa na chama hicho.

No comments:

Post a Comment