|
Ray atakayezipiga na Mhe. Zitto Kabwe |
|
Mhe Zitto Kabwe atakayepigana na Ray |
|
Mhe. Idd Azam atakayepigana na JB |
|
JB Mpinzani wa Mbunge Idd Azan |
|
Mhe Halima Mdee atakayepimana ubavu na Wolper |
|
Wolper atakayechapana na Mhe. Mdee |
|
Mhe Esther Bulaya |
|
Aunty Ezekiel |
KATIKA kunogesha Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Julai 7 kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano watapanda ulingoni kuzichapa na wasanii wa Bongo Movie.
Kwa mujibu wa Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) Yasin Abdallah 'Ustaadh' siku hiyo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe atapanda ulingoni ili kuonyeshana kazi na Vincent Kigosi 'Ray' katika pambano la raundi nne.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan yeye ataonyeshana kazi na Jacob Stephen 'JB'. wakati Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Jacklyne Wolper wenyewe watapimana ubavu, kabla ya Ester Bulaya kuchapana na Aunty Ezekiel michezo yote hiyo pia ikiwa ya raundi nne.
Ustaadh, alisema katika kuhakikisha mabondia hao hawaumizani ulingoni watavishwa vifaa maalum vya kukinga vichwa vyao ili wasipate majeraha kichwani.
Rais huyo wa TPBO alisema mara baada ya mapambano hayo ya utangulizi, itashuhudiwa michezo miwili ya kimataifa kati ya mabondia Thomas Mashali na Francis Miyeyusho kuzichapa na Wakenya Patrick Amote na Shadrack Machanje.
Pia maboindia Ramadhani Mkundi atapanda ulingoni pia kupigana na Martin Richard, huku pia ikitarajiwa kuwepo kwa burudani mbalimbali za muziki na mchezo wa soka kati ya wabunge mashabiki wa Simba dhidi ya wale wenzao wa Yanga na Bongo Fleva kuumana na Bongofleva.
Ustaadh alisema michedzo hiyo iliyoandaliwa na Global Publishers ni maalum kwa ajili ya kuchanisha fedha za ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike na kutoa wito wadhamini na watu mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangia na pia kuhudhuria tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment