STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 7, 2013

Extra Bongo yanasa wawili toka Congo kuwatambulisha siku ya Eid

 KATIKA kujiimarisha zaidi na kutaka kuendelea kufunika nchini bendi ya Extra Bongo 'Wana Next Level' maarufu kama Wazee wa Kizigo, wamewanyakua wanenguaji wapya wawili wa kike kutoka DR Congo watakaotambulishwa rasmi kwa mashabiki katika maonyesho ya sikukuu ya Eid el Fitri.
Wanenguaji hao walitambulishwa mchana wa leo kwa wanahabari ni Jolie Moncotina Kindu 'Mrinsho Ngassa' na Grace Messu Kamba (Fatuma) au maarufu kama John Bocco waliodai wanatoka katika makundi ya wanamuziki Werrason Ngiama Makanda na Ferre Golla.
Utambulisho huo ulifanyika kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki 'Kamarade' alisema wanenguaji hao tayari walioshaanza mazoezi na wasanii wenzao ila walikuwa wakisubiri vibali vya kufanya kazi nchini.
"Tumekuwa nao kwa muda wakiendelea na mazoezi wakati tukihangaikia vibali vyao na tunashukuru vibali vimepataika ana hivyo watawatambulishwa rasmi katika maonyesho yetu ya sikukuu ya Eid katika kumbi za Meeda Club-Sinza Mori na Dar Live," alisema Choki.
Aidha Choki alisema bendi yao pia itatambulisha siku hiyo kwa mashabiki wao nyimbo mbili mpya za 'Hafidh' uliotungwa na Michael Athanas 'Montanabe' na 'Mwanamke Hapigwi' Papii Catalogue.
"Pia kutakuwa na nyimbo mbili zitakazotambulishwa sambamba na zile mbili za Mgeni wa Khadija Kimobitel na Sagna nilioutunga mimi lakini anaimba sehemu kubwa Kimobitel," alisema.
Nao wanenguaji hao walioonyesha manjonjo yao kwa wanahabari, walisema wamekuja nchini kuonyesha namna ya kunengua, huku wakisema wanajiita majina ya washambuliaji hao nyota wa soka wa Taifa Stars kutokana na kukunwa na umahiri wao dimbani.
"Tangu niko kule Kin, namuonaga Murisho Ngassa namna anavyochezaga nami navutiwa na yeye ndiyo najipa hii jina yake, na nitafunika kama Ngassa," alisema Jolie ambaye angalau anakifahamu kiswahili kuliko mwenzake aliishia kusema yeye ni John Bocco tu.
Naye Rapa Catalogue alisema wimbo wake mpya una lengo la kuleta mabadiliko na utetezi kwa wanawake kutokana na mikstari yake inayoasa wanaume kutowapiga wanawake wala kuwanyanyasa badala yake iwatunze vyema ili wasije wakawaacha na kupata wanaojua kubembeleza.
"Pia kuna rapu mpya nitatitambulisha siku hiyo inayosema tutaishie Dar bila ya kazi, tutaishije Dar es Salaama bila ya kazi wakati taka, maji umeme na kila kitu lazima pesa..." alisema rapa huyo mahiri.
Kiongozi na mwalimu wa uenguaji wa bendi hiyo, Super Nyamwela alisema kutua kwa wasanii hao wawili kumeongeza chachu na kuboresha safu yao na kwamba hataki kusema mengi ila kuwataka mashabiki wajitokeze katika maonyesho yao waone kazi.
"Sitaki kusema sana kwa sababu hakuna asiyemjua Nyamwela na kazi yake, mimi ni mwalimu na mashabiki waje waone kwa nini anaitwa mwalimu, wenzetu wamezoea kuongea sasa ila mimi na bendi yangu ni watu wa vitendo zaidi," alisema Nyamwela.

No comments:

Post a Comment