WANAFUNZI wawili wa
shule ya msingi Itobo wilaya ya Nzega mkoani wa Tabora wamekufa maji
katika bwawa wakati wakiwinda bata mzinga.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Peter Ouma alisema Massanja
Shija (42) ambaye ni baba wa mmoja wa watoto hao waliokufa, amenusurika
katika tukio hilo baada ya kunasa kwenye tope.
Kamanda alitaja
watoto waliokufa ni Elias Massanja (13) na Shabani Ramadhan (15) wote
wanafunzi wa darasa la sita shule ya Msingi Itobo. Tukio hilo ni la
Julai 30 mwaka huu, saa 12:30 jioni katika Kijiji cha Chamwabo, Kata
Itobo.
Ouma alisema
walikuwa wakiwinda bata mzinga ambaye aliruka na kwenda kwenye bwawa na
katika kumfuata, walizama katika kina kirefu cha maji.
Alisema baada ya kuzama, jitihada za kuokoa miili yao ilikuwa ngumu kutokana na kukosa waokoaji. Hata hivyo baadaye iliopolewa.
Mbunge wa Jimbo la
Bukene, Selemani Zedi alisema tukio hilo ni la kusikitisha kwa jamii.
Aliwataka wananchi kuwa makini na mabwawa.
No comments:
Post a Comment