STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 19, 2013

Mourinho, Tottenham waanza vyema Ligi Kuu England

He's back: Jose Mourinho blows kisses to the Stamford Bridge crowd on his returnKocha Jose Mourinho akionesha ishara ya busu kwa mashabiki wa Chelsea waliofurika  Stamford Bridge 
Comfortable: Oscar set Chelsea going in the 13th minute and there was no way back for Hull from thereMfungaji wa bao la kwanza la Chelsea Oscar akishangilia na Torres.Easy does it: Oscar celebrates scoring the opening goal 
Oscar akishangilia bao lake
Missed: Frank Lampard saw his penalty saved by McGregor 
Mfungaji wa bao la pili la Chelsea akiwajibika uwanjani.

KOCHA wa Chelsea , Mreno, Jose Mourinho ameanza kwa kishindo  Stamford Bridge  tangu arejea kwa mara ya pili baaada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu mpya ya ligi kuu soka nchini England,  Hull City.

Ikiwa imepita takribani miaka sita tangu aondoke darajani na kurejea majira haya ya kiangazi, leo hii Mourinho alianza kibarua katika dimba la nyumbani na kushangiliwa na mashabiki lukuki wanaomuunga mkono kwa asilimia mia moja.

Katika mchezo huo, kiungo mkongwe wa Chelsea,  Frank Lampard alikosa mkwaju wa penati  dakika ya sita baada ya kipa wa Hull,  Allan McGregor kuokoa na baada ya hapo kipa huyo aliokoa tena mpira wa kichwa uliozamishwa na  Branislav Ivanovic , lakini teknolojia ya goli iligoma na kuwaambia Chelsea sio goli.

Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na Oscar katika dakika ya 13 akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa Kevin de Bruyne, na bao la pili limefungwa na Frank Lampard dakika ya 25 na kufuta makosa ya kukosa penati.
Katika pambano jingine ;a mapema jana, Tottenham wakiwa ugenini waliipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Bao pekee lililoipa vijana wa Spurs ushindi huo lilifungwa na mchezaji mpya wa timu hiyo Roberto Saldado kwa njia ya penati dakika ya 50.

No comments:

Post a Comment