STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, November 22, 2013

Maguli aomba sapoti nje ndani Kili Stars ibebe Chalenji Kenya

Elias Maguli
MSHAMBULIAJI mpya na chipukizi wa timu ya taifa ya Kilimanjaro Stars, Elias Maguli, amewaomba watanzania waliopo Kenya na wale wa nyumbani Tanzania kuwaunga mkono katika ushiriki wao wa michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza Jumatano nchini humo.
Maguli alisema kwa watanzania wanaobaki nyumbani waiunge mkono timu hiyo kwa kuiombea dua na kuifanyia maombi, huku wale wa wanaishi Kenya kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwashangili ili timu hiyo ifanye vyema katika michuano hiyo inayoshirikisha timu za nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Akizungumza na MICHARAZO mchana huu katika mahojiano maalum, Maguli anayeichezea Ruvu Shooting na kushika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, alisema bila kuungwa mkono ni vigumu Kili Stars kufanya vyema katika michuano hiyo.
Maguli alisema wachezaji wa kikosi hicho kinachotarajiwa kuondoka Jumatatu kabla ya Alhamisi kuwavaa Chipolopolo ya Zambia wamejiandaa vya kutosha kuwapa raha watanzania kutokana na maandilizi waliyofanya chini ya kocha wao, Kim Poulsen, lakini sapoti ya mashabiki ni muhimu.
"Wachezaji tumejiandaa vya kutosha kutowaangusha watanzania, nasi tunaomba tuungwe mkono kwa wlaiopo Kenya wajitokeze uwanjani na wale wa nyumbani watuunge mkono kwa sala na maombi na hatimaye tutarejea na kikombe Mungu akipenda," alisema.
Kuhusu kuwemo kwenye kikosi hicho cha Kili Stars, Maguli alisema anajisikia fahari kwa kuwa Tanzania ina wachezaji bora na nyota lakini kocha amemuona anastahili kuiwakilisha nchi na atapigana kiume akishirikiana na wenzake ili kuipa timu hiyo taji lake la nne.
Tanzania Bara imenyakua ubingwa wa michuano hiyo mwaka 1974, 1994 na 2010 na mara nyingine zote tangu michuano hiyo ianze kutambuliwa kama Chalenji miaka 40 iliyopita imekuwa kama msindikizaji tu.

No comments:

Post a Comment