STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 17, 2013

Uchaguzi wa Simba kufanyika Januari


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage
MWENYEKITI wa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden Rage ameibuka na kufafanua baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakielekezwa kwake hasa sakata la kusajiliwa kwa Emmanuel Okwi na mahasimu wao Yanga na kuweka bayana ili kuondoa mzozo wa fitina Msimbazi, huenda akautisha uchaguzi mkuu Januari.
Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, uchaguzi mkuu wa klabu hiyo unatakiwa kufanyika Mei mwakani, lakini kwa vile hali inaonekana tete ndani ya klabu hiyo Mwenyekiti huyo alisema amekutana na viongozi wa matawi na kuzungumza nao na kutoa pendekezo la kuitiosha uchaguzi mkuu mapema tofauti na unavyotakiwa.
"Nimekutana nao na lengo kuu ni kuzungumza hali iliyopo ndani ya klabu na kama tatizo ni mimi basi nipo tayari kuitisha uchaguzi hata Januari ili Simba iingie duru la pili ikiwa na amani na utulivu na iliyokamilika safui mpya ya uongozi kwa maana ya Mwenyekiti, Makamu na Kamati ya Utendaji mpyam," alinukuliwa Rage.
Rage alisema kuwa tofauti yake na wenzake ni msimamo wake wa kupigania haki za klabu na hasa kutaka kila kitu kifanyike klabu na kwa uwazi.
Kuhusu sakata la Okwi analotupiwa lawama kwamba alisaidia kutua kwake Jangwani, Rage alisema ni kutaka kumbebesha lawama usiomhusu kwani kwa kipindi kirefu akikuwa nje ya nchi na kama Okwi alikuwa ni muhimu Simba Kamati ya usajili ingemsajili kama ilivyofanywa kwa wachezaji wengine watatu.
Kamati hiyo ya Simba imewasajili makipa Ivo Mapunda, Yew Berko na beki wa Gor Mahia, Donald Musoti na Rage alihoji mbona hao walisajiliwa na vipi Okwi asingesajiliwa na badala ya wanachama kumtupia lawama zisizo na maana yoyote.
Wanachama wa Simba wakiongozwa na tawi la Mpira Pesa limekuwa likimshutumu Rage kuhusu suala la Rage kwamba aliwacheza shere na kuapa kwamba wangeenda nyumbani kwake mara baada ya pambano lap na Yanga na Nani Mtani Jembe siku ya jumamosi kushinikiza kujiuzulu au kuzionyesha fedha za usajili za mchezaji huyo aliyeuzwa Etoile du Sahel ya Tunisia kabla ya kurejea kwao Sc Villa Yanga ilipoenda kumnasa.
Kuhusu uchaguzi huo ujao, Rage alisema hana mpango wa kuwania nafasi yoyote katika klabu hiyo na hasa kutokana na kuchoshwa na vurugu ndani ya Simba ambazo zimemlenga yeye binafsi kila mara hasa mtu mmoja tu aliyemtaja kuwa hohehahe.
"Sintagombea uongozi wala kutetea kiti changu, ili kuachia wengine waiongoze Simba iwapo kama mimi ni tatizo," alisema Rage na kusisitiza kuwa fedha za Okwi hazijalipwa na wala hazijalipwa hivyo wanachama wa Simba watulie.

No comments:

Post a Comment