STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 22, 2014

Manchester City yaua ikitinga Fainali Kombe la Ligi, Utd kazi leo

MABAO matatu yaliyowekwa kimiani na Alvaro Negredo aliifungia mawili na Sergio kun Aguero yaliiwezesha Manchester City kufuzu Fainali ya Kombe la Ligi (Capital One) dhidi ya West Ham United.
City licha ta kucheza ugenini iliendeleza wimbi lake la ushindi mfululizo na kuonyesha kiu yake ya kutaka kunyakua mataji manne kama ahadi ya kocha wake Manuel Pellegrini.
Kwa ushindi huo wa jana , City imeing'oa West Ham kwa jumla ya mabao 9 kwani katika pambano la awali lililochezwa uwanja wa Itihad, wakali hao waliitandika mabao 6-0.
Sasa inasubiri mshindi wa mechi ya marudiano ya nusu fainali ya michuano hiyo kati ya Manchester United dhidi ya Sunderland.
Katika mechi yao ya kwanza United walikandikwa mabao 2-1 na hivyo kulazimika leo kushinda ili kutinga fainali angalau kujiwekea hai matumaini ya kunyakua taji kwa msimu huu baada ya kuwa na wakati mgumu kwenye Ligi Kuu na huku ikiwa imeondoshwa FA.

No comments:

Post a Comment