STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 22, 2014

Twiga Stars kuvaana na Zambia ugenini Feb 15


Na Boniface Wambura
TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ itaivaa Zambia katika mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano ya mchujo ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayofanyika Februari 15 mwaka huu jijini Lusaka.
Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Nkoloma kuanzia saa 9 kamili kwa saa za Zambia na itachezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga kutoka Rwanda.
Mukansanga atasaidiwa na Wanyarwanda wenzake; Francine Ingabire, Sandrine Murangwa na Angelique Tuyishime. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jackey Gertse kutoka Namibia.
Wakati huo huo: Shrikisho la Soka Afrika (CAF) limeteua Watanzania Alfred Rwiza Kishongole na Lina Kessy kuwa makamishna wa mechi za shirikisho hilo zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 mwaka huu.
Kishongole ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Cote d’Or ya Shelisheli na Kabuscorp de Palanca ya Angola.
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mchujo itafanyika Shelisheli na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Abdoul Ohabee Kanoso. Waamuzi wengine ni Basile Alain Rambeloson, Augustin Gabriel Herinirina na Andofetra Avombitana Rakotojaona.
Naye Kessy atakuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Rwanda na Kenya itakayochezwa jijini Kigali.
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Cameroon. Mwamuzi wa kati ni Sylvie Abou wakati wasaidizi wake ni Winnie li Koudangbe, Lum Rochelle na Jeanne Ekoumou.

No comments:

Post a Comment