MABINGWA wa soka nchini, Azam Fc, imesema kiungo wake Frank Domayo atakuwa nje ya uwanja wa muda wa
miezi minne kufuatia upasuaji wa mguu aliofanyiwa nchini Afrika Kusini.
Akizungumzia jiji Afisa Habari wa Azam, Jaffar Idd amesema
uchunguzi wa afya wa kiungo huyo aliofanyiwa na mganga mkuu wa klabu
hiyo Dk Mwamkemwa ulibaini kuwa Domayo ana matatizo ya msuli wa mguu
wake wa kushoto na kwamba atatakiwa kufanyiwa upasuaji.
Domayo alipekwa na uongozi
wa Azam wiki iliyopita nchini Afrika Kusini
akiambatana na Dk Mwankemwa ambapo juzi alifanyiwa upasuaji katika
hospitali ya Vicent Parent na imeelezwa kuwa anaendelea vizuri huku
akitarajiwa kurejea nchini Jumapili.
Afisa Habari huyio amesema kiungo huyo atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi
miezi minne akiendelea kupata tiba na uangalizi wa karibu wa jeraha lake
kabla ya kurejea uwanjani kuitumikia klabu yake hiyo mpya ambayo
amejiunga nayo hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment