Waflame wa soka Afrika, Ivory Coast |
Oyooooooooooooooooo! |
Nahodha Yaya Toure akipokea Kombe toka kwa Rais Nguema |
Katika fainali za mwaka huo, Ghana maarufu kama Black Stars walikufa kwa mikwaju ya penati 11-10 na usiku wa kuamkia leo walikubali tena kipigo cha penati 9-8 kwa wapinzani wao na kuliacha taji likienda kwa Ivory Coast ikiwa ni mara ya pili kwao.
Timu hizo zililazimika kupigiana penati baada ya kumaliza dakika 120 bila ya kufungana na katika upigaji wa penati, Ivory Coast walianza vibaya kwa Wilfried Bony kukosa penati, lakini haikuweza kuwakatisha tamaa Tembo wa Afrika kumaliza udhia na ukame wa miaka zaidi ya 20 tangu wanyakue taji la kwanza 1992.
Ghana wanaweza kujilaumu kwa kushindwa kuibuka mabingwa kwa mara ya tano kutokana na kipindi cha pili cha dakika 90 kutawala sehemu kubwa ya pambano hilo lililosisimua kutokana na lilivyokuwa kali.
Katika hatua ya mikwaju ya penati Black Stars walianza kwa Mubarak kufunga kabla ya Bony kukosa, Jordan Ayew akapata penati ya pili ya Ghana na Tallo wa Ivory Coast naye akaikosa penati yake na kufanya matokeo kuwa 2-0.
Hata hivyo Acquah na Acheampong walikosa penati zilizofuata za Ghana, wakati Aurierna Doumbia walifunga zao na matokeo kuwa 2-2.
Andre Ayew alifunga mkwaju wake na Yaya Toure akasawazisha, John Mensah akafunga na Solomon Kalou akasawazisha kabla ya Agyemang-Badu kufunga mkwaju wake na Koro Toure kusawalisha.
Afful aliifungia Ghana na Kanon kusawazisha zoezi likawa piga nikupige hadi katika penati ya tisa ambapo Ghana kupitia kipa wake Razak Brimah ilikosa na Ivory Coast kutumbukiza yao iliyowapa ubingwa wa pili katika historia za michuano hiyo kupitia kwa Boubacar Barry aliyegeuka kuwa shujaa kabla ya nahodha Yaya Toure kukabidhiwa taji na Rais wa Guinea ya Ikweta, Nguema kwenye uwanja wa Bata.
No comments:
Post a Comment