STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 9, 2015

Irene Uwoya awataka mashabiki wake kupokea Kisoda

Na Rahma White
MUIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Irene Uwoya 'Oprah' amewataka mashabiki wake kujiandaa kuipokea kazi yake mpya iitwayo 'Kisoda' akidai ni kazi kali kuliko hata filamu yake ya awali iitwayo 'Apple' aliyoitoa mwaka jana.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Irene alisema 'Kisoda' ni moja ya kazi zitakazoleta mapinduzi makubwa katika fani ya uigizaji nchini kwa namna ilivyoandaliwa ikishirikisha wasanii wa ndani na nje ya nchi.
Irene alisema filamu hiyo iliyomtafuna fedha nyingi ipo katika hatua ya uhariri na itaachiwa wakati wowote zoezi hilo likikamilika akiwataka mashabiki wajiandae kuipokea kwa mikono miwili.
"Kama kuna waliodhani nilibahatisha kwenye 'Apple', wamekosea safari hii naja na 'Kisoda', moja kati ya filamu kali ambayo imewashirikisha wasanii wa Tanzania na Afrika Kusini, chini ya kampuni yangu ya Apple Entertainment," alisema Irene.
Msanii huyo alisema amekusudia ndani ya mwaka 2015 awape burudani ya kutosha mashabiki wake na kwa kuanza ameanza na Kisoda kabla ya kufuatiwa na mambo mengine makubwa zaidi.
Irene aliwataja baadhi ya wasanii walioshiriki filamu nchini wa hapa nchini ukiondoa yeye (Irene) ni Islam, Mariam Ismail na Msami.
Kimwana huyo aliyewahi kunyakua tuzo ya Muigizaji w Kike Chipukizi wa tuzo za Kinara kupitia filamu ya Diversion of LOve' kabla ya kuanza kuzalisha filamu zake na kuwahi  kuendesha kipindi cha kwenye runinga cha 'Paradise Show' ameshiriki filamu zaidi ya 30 zilizomjengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya kazi hizo ni; 'Ngumi ya Maria', 'Nyati',  'Zawadi Yangu', 'Aliyemchokoza Kaja', 'Figo','Rosemary', 'Snitch', 'The Return of Omega', 'Money Talk', 'Omega Confusion', 'Question Mark', 'Safari', 'Innocent Case', 'Nyota Yangu', 'Last Card', 'Doa la Ndoa', 'Offside' na 'Oprah'.

No comments:

Post a Comment