STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 3, 2015

Shamsa Ford ataka ubunifu zaidi Bongo Movie

WASANII waigizaji nchini wameaswa kuwa wabunifu na kuumiza vichwa kutengeneza kazi za kipekee ili kujitofautisha na pia kulenga kujitangaza kimataifa.
Wito huo umetolewa na muigizaji nyota nchini Shamsa Ford ambaye amesema bila ubunifu na kutoa kazi za kipekee ni vigumu wasanii watanzania kujitangaza katika anga la kimataifa.
Shamsa alisema hata yeye alifikiria na kujaribu kuibuka kivyake vyake katika simulizi la 'Chausiku' ambayo imemjengea jina hata kwa wale ambao siyo mashabiki wa filamu.
"Ubunifu ndiyo siri ya mafanikio, hata mimi niliumiza kichwa kuja na filamu ya 'Chausiku' kwa nia ya kujitofautisha na ninashukuru kazi ilipokelewa vema kiasi kwamba kwa sasa nimepata changamoto ya kutoa kazi nyingine itakayovutia kama hiyo au zaidi," alisema.
Shamsa alisema kwa kuonyesha hakubahatisha kwa sasa yupo katika maandalizi ya kuja na filamu ya 'Mama Muuza' ambayo imebeba uhalisia wa maisha ya uswahili yaliyozoeleka.
"Hakuna njia ya mkato katika mafanikio na hata soko la kimataifa ni ubunifu na kutoa kazi ya kipekee, ili hata zikishindanishwa ijitofautishe," alisema Shamsa.

No comments:

Post a Comment