STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 5, 2012

Afisa Habari KIFA afia ofisini



AFISA Habari wa chama cha soka Manispaa ya Kinondoni (KIFA), Seif Mairo 'Saddam', alifariki dunia jana baada ya kuanguka ghafla akiwa kwenye ofisi za chama hicho.
Taarifa za kifo chake ziliwasilishwa na Mweka Hazina wa KIFA, Harid Kamguna.
Kamguna alisema Mairo aligundulika kuwa tayari amefariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Alisema Afisa habari huyo mwenye umri wa miaka 76 anatarajiwa kuzikwa leo mchana katika makaburi ya Ndugumbi jijini Dar es Salaam.
Alisema marehemu alianza kazi hiyo tangu mwaka juzi na alisifiwa kwa ushirikiano wake mzuri na vyombo vya habari.
Enzi za uhai wake Mairo, aliyekuwa akifahamika zaidi kama Saddam, mbali na kuucheza mpira katika timu mbalimbali pia amewahi kuziongoza klabu kadhaa pamoja na soka la kuendeleza vipaji vya watoto na vijana kupitia chama cha Kinondoni, KIDYOSA na ni mmoja wa waasisi wa chama cha yosso cha Dar, DAYOSA aliyowahi kuwa Katibu Msaidizi kwa kipindi kirefu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa chama hicho.
Kamguna alisema marehemu ameacha mke na mtoto mmoja. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen.

Chanzo:NIPASHE

No comments:

Post a Comment