STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, March 29, 2013

Goti lamtia hofu Zahoro Pazi


MSHAMBULIAJI wa timu ya JKT Ruvu, Zahoro Pazi ameingiwa hofu na jeraha la goti alilopata wakati wa pambano lao dhidi ya Polisi Morogoro huenda ikamvurugia mipango ya safari yake ya kurejea Afrika Kusini kujaribu kuchezas soka la kulipwa.
Pazi ametakiwa kurejea tena nchini humo Mei mwaka huu kulingana na makubaliano yake na klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini Bloemfotein Celtic, iliyomfanyia majaribio ya kuichezea yaliyofanyika Januari mwaka huu.

Hata hivyo mchezaji huyo alisema ameanza kupatwa hofu baada ya kupata maumivu makali alipoumia kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Moro, pambano lililoisha kwa JKT Ruvu kushinda mabao 3-2.
Akizungumza na MICHARAZO, Pazi alisema pamoja na uvimbe uliokuwapo katika goti hilo kuisha bado anahisi maumivu makali kwa ndani japo linalomnyima raha, ingawa alisema benchi la utabibu la klabu yake linamshughulikia vyema.
"Haya maumivu ya goti niliyonayo yananikatisha tamaa, nashindwa kuitumikia klabu yangu na wakati huo huo nina mwezi mmoja tu wa kujiandaa kabla ya kurejea Afrika Kusini kuendelea na majaribio yangu klabu ya Bloemfotein Celtic," alisema Pazi.
Mtoto huyo wa kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Idd Pazi 'Father' anayeichezea JKT kwa mkopo akitokea Azam, alisema anatamani apone haraka goti hilo ili ajifue zaidi kusudi akienda Afrika Kusini awaridhishe mabosi wa Bloemfotein.

No comments:

Post a Comment