STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, March 29, 2013

Humud apaa zake kwenda Jomo Cosmo



KIUNGO mahiri wa timu ya Azam, Abdulhalim Humud 'Gaucho' ameondoka nchini asubuhi hii kuelekea Afrika Kusini kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika kalbu ya Jomo Cosmo.
Meneja wa klabu ya Azam, Patrick Kahemele aliiambia MICHARAZO mapema leo kuwa, Humud
atakuwa nchini humo kwa muda wa siku 10 akifanyiwa majaribio na klabu hiyo  inayopigana kutaka kurejea kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).
Kahemele alisema Humud ameenda Afrika Kusini ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya klabu yao ya Azam ya kupanua wigo wa wachezaji wa kitanzania kucheza soka nje ya nchi kwa manufaa ya nchi siku za baadaye.
"Humud ameondoka asubuhi hii (jana) kuelekea Afrika Kusini kufanyiwa majaribio katika klabu ya Jomo Cosmo na atakuwa huko kwa siku 10 kabla ya kurejea nchini" alisema Kahemele.
Klabu hiyo ya Cosmo inamilikiwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) Jomo 'Black Prince' Sono, na iwapo Humud atafaulu majaribio yake atafuata nyayo za wachezaji wa Kitanzani kuwahi kuichezea timu hiyo akitanguliwa na nyota wa zamani  Nteze John na Ally Shah kuwahi kufanya hivyo miaka ya nyuma.

No comments:

Post a Comment