STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 24, 2013

Kamati ya Utendaji Simba yamaliza mzozo wa makocha wao


Makocha wa Simba, Julio na Liewig waliosuluhishwa na kamati ya utendaji ya Simba
KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba imemaliza mzozo uliokuwepo kati ya makocha Patrick Liewig na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelu 'Julio' baada ya kuwakutanisha na kutoa maamuzi katika kikao chao kilichofanyika jana.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani za klabu hiyo zinasema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa kamati hiyo kuliweka sawa benchi lake la ufundi kutokana na makocha hao kubwatukiana kwenye kikao kila mmoja akitaka kuwa juu ya mwenzie.
Chanzo cha habari ndani ya Simba kiliiambia MICHARAZO kuwa, licha ya majibizano yaliyoibuka kwenye kikao hicho, lakini mwishoe ilitolewa maamuzi kwamba Liewig ndiye anayepaswa kusikilizwa kama kocha mkuu na wasaidizi wake wakipaswa kumtii kwa manufaa ya klabu yao.
"Kikao kikubwa kizito kutokana na makocha hao kubwatukiana mbele yetu kabla ya kuwaweka sawa na kuwasuluhisha ambapo maamuzi yaliyofikiwa ni kwambna maamuzi yote katika timu yafanywe na kocha mkuu peke yake na wasaidizi ni kufuata baadaye ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima," chanzo kilisema.
Pia kikao hicho kiliamua kwa pamoja kwa kukubaliana na benchi lao la ufundi kuiingiza timu kambini huko Bamba Beach kwa ajili ya pambano lao la kesho dhidi ya Ruvu Shooting na kwa mechi nyingine zilizosalia kza Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni huku wenyewe wakiwa wameshatemesha ubingwa.
Makocha Mfaransa Patrick Liewig na Julio waliingia kwenye mzozo baina yao kutokana na kile kilichoelezwa kutofautiana na kusababisha kuigawa timu jambo lililohatarisha klabu yao ambayo ipo nafasi ya nne kwa sasa ikiwa na pointi zake 36 ikisaliwa na mechi tatu.

No comments:

Post a Comment