STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 22, 2013

Kanali Massawe kubariki tamasha la Shule ya Jitegemee

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjc59WQhmrJFoeTwPvXXDnRfA8QPRV8naJYCW6jN7JDZshLo8ZVROyO0aKzyMDfsx56FKcsC0hglqLW3JIL3FYEsEU6Qyr7FgphtWSyhuV_aqWmjh19xt8qq-cpmQSAoTUoRjdhX2nUkc8s/s1600/RCC.jpg
RC Kanali Fabian Massawe


MKUU wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la wadau mbalimbali waliosoma Shule ya Sekondari Jitegemee ya jijini Dar es Salaam litakalofanyika Aprili 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari shuleni hapo jana, Mkuu wa Shule hiyo, Kanali Martin Mkisi, alisema wamemwalika Kanali Massawe ambaye amewahi kuiongoza shule hiyo, ili aweze kupata fursa ya kukutana na wadau wa shule hiyo kujadili changamoto mbalimbali.

Alisema pamoja na mambo mengine, wataendesha harambee, ambayo wanatarajia kukusanya sh milioni 50 ili kuiendeleza shule hiyo na fedha zitakazopatikana zitasaidia kumalizia ujenzi wa ukumbi ambao umeanza kujengwa kama moja ya harakati za kukabiliana na changamoto zinazoikabili Jitegemee Sekondari.

Kanali Mkisi alisema hakutakuwa na kiingilio, hivyo amewaalika wadau na marafiki wa shule hiyo kuhudhuria kwa wingi, ili kuliwezesha kufana na huo utakuwa mwendelezo wa matamasha ya namna hiyo kila mwaka.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya tamasha hilo, Masemele Masemele, alisema tamasha hilo litahusisha michezo mbalimbali, ukiwemo mpira wa wavu, kikapu, kuvuta kamba pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama vile Mh. Temba na wengineo.

No comments:

Post a Comment