STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 27, 2013

Machupa, Kisiga waibeba Golden Bush wakiipa kichapo Wahenga Fc

Shaaban Kisiga (Katikati) akiwatoka wachezaji wa Wahenga Fc

Nyota wa Wahenga Fc, Macocha Tembele akiwatok wachezaji wa Golden Bush

Yusuf (9) wa Wahenga, akitafuta mbinu za kumtoka Abuu Ntiro huku wachezaji wenzake wakiwa tayari kumpa msaada katika pambano lao lililochezwa jana na Wahenga kunyukwa mabao 2-1

Abuu Ntiro akimtoka Yusuf

Heka heka katika lango la Wahenga Fc

NYOTA wa zamani wa Simba na taifa Stars, Athuman Idd Machuppa na Shaaban Kisiga 'Marlon' jana waliisaidia Golden Bush Veterani kupata ushindi muhimu  wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Wahenga Fc katika pambano maalum la kusherehekea  Miaka 49 ya Muungano.
Timu hizo zilipambana katika mchezo mkali na uliosisimua uliochezwa kwenye uwanja wa TP Afrika, Sinza Darajani, ambapo Machuppa, Kisiga wakisaidiwa na nyota wa zamani wa Simba na Yanga walifunga mabao hayo katika muda wa dakika tano tu mara baada ya kurejea toka mapumziko timu zikiwa hazijafungana.
Machuppa ndiye aliyeanza kuifungia Golden Bush bao tamu katika dakika ya 68 akimalizia kazi nzuri ya Herry Morris kabla ya Kisiga kuongeza jingine dakika tano baadaye na kuzima matumaini na Wahenga Fc waliokuwa uwanja wa nyumbani kulipa kisasi ilichokutana nacho mwezi uliopita kwenye uwanja wa Kinesi.
Katika pambano hilo la Kinesi, Wahenga walinyukwa pia mabao 2-1 huku mvua ikiwanyeshea timu zote mbele ya aliyekuwa mgeni rasmi, Kamanda wa Polisi, Thobias Andengenye.
Golden Bush na kikosi kilichosheheni nyota waliowahi na wanaendelea kutamba nchini kama kipa Aman Simba, Abuu Ntiro, Godfrey Bonny 'Ndanje', Wisdom Ndlovu, Herry Morris, Said Sued, Salum Sued, Kisiga, Machuppa na wengine waliifanya Wahenga ishindwe kufuruka licha ya mara kadhaa kubisha hodi langoni mwa mwao.
Dakika chache kabla ya pambano hilo kumalizika huku kiza kikiwa kimeshaanza kutamba uwanjani, Wahenga walipata bao la kufutia machozi lililofungwa kwa mkwaju wa penati na nyota wa kikosi hicho, Macocha Tembele aliyekuwa akihaha uwanja mzima kuibeba timu yake.
Licha ya Wahenga kuendelea kushambulia lango la Golden Bush, mpaka kipyenga cha mwamuzi, Pondamali kulia walijikuta wakiendelea kuwa 'wateja' wa Wakali wa soka Dar es Salaam kwa kukubali kipigo kingine cha mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment