STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 13, 2013

Yanga yaitemesha Simba ubingwa, yaikwangua JKT Oljoro 3-0

Vinara wa ligi kuu Yanga walioivua Simba taji jioni ya leo
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imeendelea kudhihirisha wamepania kutwaa taji la msimu huu baada ya jioni hii kuikwangua JKT Oljoro ya Arusha mabao 3-0 katika pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo uliopatikana kwa mabao ya kipindi cha kwanza yameifanya Yanga kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 52 na kuivua rasmi Simba ubingwa kutokana na kufikisha pointi 52 ambazo haziwezi kufikiwa na Wana Msimbazi.
Simba ambayo itashula kesho dimbani kuumana na Azam yenyewe ina pointi 35 na kama itashinda mechi zake zote itafikisha pointi 50 tu.
Mabao yalioifanya Yanga kulishika taji la ubingwa kwa mkono mmoja na kusubiri mwingine iwapo Azam wanaowafukuzia watateleza katika mechi zake yaliwekwa kimiani na beki Nadir Haroub 'Cannavaro' katika dakika ya 5 tu ya mchezo kabla ya Simon Msuva kufunga la pili dakika ya 19 na Hamis Kiiza 'Diego' kuongeza la tatu dakika mbili kabla ya mapumziko.
Pambano hilo lililochezeshwa na mwamuzi Amon Paul wa Mara lilihuhudia kadi kadhaa za njano zikitolewa kwenye mchezo huo na mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga walikuwa wababe mbele ya maafande hao kwa ushindi huo wa mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment