STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, May 16, 2013

Beckham astaafu soka, Lampard akomaa Chelsea

David Beckham

Frank Lampard akiwa na taji la Europa ililotwaa Chelsea usiku wa jana
WAKATI nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England, David Beckham akitangaza kustaafu rasmi soka siku chache baada ya kufanikiwa kuiwezesha PSG kunyakua taji la Ligue 1 baada ya miaka 19 mwishoni mwa wiki, kiungo nyota wa Chelsea, Frank Lampard yeye ameongeza mkataba mpya na klabu yake hiyo.
Beckham amenukuliwa kuwa atatundika rasmi daluga zake mara baada ya pambano la kufungia msimu la timu yake hiyo aliyoichezea kwa mkataba wa mwaka mmoja, itakaposhuka dimbani Mei 26.
Mkali huyo aliyewahi kutamba na timu kadhaa kama Manchester United, Real Madrid na LA Galaxy ambako kote huko alkiweza kunyakua matji ya ligi ya nchi hizo.
Kustaafu kwa Beckham aliyeichezea timu ya taifa jumla ya mechi 115 na kuifungia mabao 17, ameishukuru klabu ya PSG kwa kumpa nafasi ya kujiunga nayo na kusema kuwa anadhani ni muda muafaka wa yeye kupumzika baada ya kucheza soka kwa kiwango cha juu.
Nyota huyo aliyekuwa mahiri kwa mipira ya faulo, amemshukuru kocha Carlo Ancelloti na wana PSG kwa ujumla kwa muda aliokuwa nao na kuisaidia timu hiyo kufika ilipofikia kwa kunyakua taji hilo la Ligi ya Ufaransa.
Wakati Beckham akitangaza kung'atuka akimfuata aliyekuwa kocha wake wakati akiichezea Manchester United, kiungo mwingine mkongwe wa England, Frank Lampard amesaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja baada ya tetesi kwamba angeondoka klabu hapo kwenye kucheza Ligi Kuu ya Marekani (MSL).
Taarifa zilizotangaza jioni hii zinasema kuwa Lampard amesaini mkataba huo saa chache baada ya kuisaidia Chelsea kunyakua taji la Ligi Ndogo ya Ulaya na siku chache tangu aweke rekodi ya ufungaji mabao katika klabu hiyo ya 'Darajani'.
"Napenda kumshukuru Roman Abramovich kwa kunipa nafasi ya kuitumikia klabu ninayoipenda kwa dhati ya Chelsea, pia wachezaji wenzangu, maafisa wote wa timu hii na wote wanaoiunga mkono Chelsea kwa namna walivyonipokea na kuishi nami tangu nilipotua kwa mara ya kwanza," alinukulia Lampard.
Mkataba wa mchezaji huyo ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimui na kulikuwa na taarifa kwamba alikuwa tayari kuondoka kuelekea Marekani kufuatiwa kuonyesha kutohitajiwa tangu alipotua timu ilipokuwa chini ya AVB anayeinoa Tottenham Hotspur kabla ya rafa Benitez kumpa nafasi na kuvunja rekodi ya ufungaji wa maboa klabu hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment