STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 12, 2013

Golden Bush Veterani watepeta tena kwa vijana wao walambwa 3-1

Hiki ndiko kikosi cha Golden Bush Fc kinachowanyanyasa wazee wao kila wanapokutana katika mechi za kujipima nguvu. Wa kwanza kulia (waliosimama) ni kocha wao, Katina Shija na mwishoni ni Meneja wao Wazir Mahadhi 'Mandieta'.
WAKALI wa soka la veterani jijini Dar es Salaam, Golden Bush imeendelea kuwa 'urojo' na kushindwa kabisa kupata 'tiba' ya kuepuka vipigo toka kwa vijana wao wanaoshiriki Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Kinondoni, Golden Bush FC baada ya asubuhi ya leo kukubali kipigo kingine cha mabao 3-1.
Hicho ni kichapo cha pili mfululizo kwa Veterani hao toka kwa vijana wao baada ya mwezi uliopita kunyukwa mabao 2-1.
Katika pambano la asubuhi ya leo 'wazee' hao wanaowatumia nyota wa Simba na Yanga walishindwa kuwazuia vijana wao na kukubali kipigo hicho kilichotokana na mabao ya Ayoub Lipati na Ibrahim Ramadhani aliyetumia mawili kabla ya Kudra Omar, kuipatia Golden Bush Veterani bao la kufutia machozi.
Mlezi na Msemaji wa timu ya wazee, Onesmo Waziri 'Ticotico' amekiri kwamba kikosi chake kimeshindwa kupata dawa ya kuwadhibiti vijana wao walioimarika zaidi kwa sasa huku wakiongoza msimamo wa kundi lake katika Ligi ya TFF-Kinondoni..
"Hawa vijana hatuwazi tena maana wanatufanya watakavyo kama tunavyowanyanyasa watani zetu Wahenga Fc. Wameimarika sana kwa sasa," alisema Ticotico ambaye hucheza kama mshambuli wa pembeni.

No comments:

Post a Comment