STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 12, 2013

Real Madrid wateja taji la Ligi Kuu Hispania, Barca wapeta kilaini

Christian Stuani Cristiano Ronaldo of Real Madrid CF duels for the  Christian Stuani of RCD Espanyol during the La Liga match between RCD Espanyol and Real Madrid CF at Cornella-El Prat Stadium on May 11, 2013 in Barcelona, Spain.
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo akiwania mpira na mchezaji wa Espanyol jana
MABINGWA wa zamani wa Ulaya, Barcelona inayojiandaa kujitupa ugenini mjini Madrid kupambana na wenyeji wa Atletico Madrid, imewavua rasmi ubingwa wapinzani wao wa jadi Real Madrid, baada ya vijana hao wa Jose Mourinho kulazimishwa sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Espanyol.
Barcelona imetwaa taji hilo kwa kufikisha pointi 88 ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani hao hata kama watashinda mechi zao mbili walizonazo mkononi kwa sasa.
Real Madrid waliokuwa watetezi wa taji hilo kwa sare ya jana wamefikisha pointi 81 na wakishinda mechi zao zilizosalia watafikisha pointi 87 tu ambazo zimeshapitwa na Barca walio na michezo minne mkononi.
Vijana wa Mourinho walilazimika kusawazisha bao katika kipindi cha pili baada ya wenyeji wao kuwatangulia kwa bao la dakika ya 23 lililofungwa na Mruaguay Cristhian Stuani.
Bao hilo la kusawazisha la Madrid liliwekwa kimiani na Muargentina Gonzalo Higuain akimalizia kazi ya kiungo nyota wa Croatia, Luka Modric.

No comments:

Post a Comment