MWANAMUZIKI mahiri nchini wa muziki wa kizazi kipya na kiongozi wa bendi yenye mvuto nchini  ya ‘Machozi’,  Judith Wambura ( Lady Jay Dee) au  Jide ama #Teamaanaconda#,  anatarajia kuripoti Mahakama ya Kinondoni siku ya Jumatatu Mei 13, kufuatia kufikishiwa kwa taarifa hizo Gadna G Habash ‘Captain’ ambaye ni Meneja na mume wa Lady Jay Dee.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana mchana, Gadna amesema ni kweli wamepata taarifa za kutaarifiwa kwa Lady Jay Dee kufika Mahakama ya Kinondoni, siku ya Jumatatu.
“Ni kweli tumepata wito na Mahakama ya Kinondoni,  Hii ni kufuatia kwa jana  kufika watu ambao walijielezea kuwa wanatoka Mahakama hiyo na walikuja na barua ya kumkabidhi Lady Jay Dee mwenyewe hata hivyo hawakumkuta” amesema Gadna.
Ameendelea kueleza kuwa, hata alipowaeleza watu hao wamkabidhi yeye hiyo barua watu hao walisema ilikuwa si rahisi zaidi alitakiwa akabidhiwe mlengwa, hivyo kumueleza kuwa wito wa kufika mahakamani siku ya Jumatatu, na  aliwakubalia kwa hilo.
Hata hivyo, Gadna amesema hajajua Lady Jay Dee anaitiwa nini na kwa sababu ya nini amemwelezea na amesema watatekeleza wito huo wa kufuka Jumatatu Mahakamani hapo.
Aidha, kupitia kwenye ukurasa wake wa Kijamii wa facebook,  Lady Jay Dee aliandika: “Ratiba ya Usiku wa leo,  ni Machozi Band, kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea…” aliandika Jide  kwenye ukurasa huo ambao mpaka hatua ya mwindishi anatembelea ‘post’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ambayo watu mbalimbali walipata kuchangia.
Maoni hayo yanayokaribia zaidi ya 558 na, ‘Like’ zaidi ya 756 na ‘Share’ zaidi ya 20,  ambapo wengi wao wameweza kumuhusisha moja kwa moja na Mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba kuwa ndie aliyefanya hivyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali na moja ya gazeti hivi karibuni ilimnukuu Ruge kuwa amejiandaa kuchukua hatua  ikiwemo ya kisheria dhidi ya Lady Jay Dee baada ya kumsema kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
Aidha, katika kuelekea shoo yake ya Miaka 13 ya Lady JayDee, amemtangaza rasmi msanii machachari wa bongo fleva, Juma Nature.
Jide amesema Nature ameongezeka katika list ya wasanii watakaokuwepo kushiriki miaka 13  ambapo ataungana na wasanii wengine wengi siku hiyo  ambapo tayari tiketi zimeanza kuuzwa. “Naomba mujitokeze kwa wingi na tiketi zinapatikana karibu sehemu zote ikiwemo Shear Illusions Mlimani City, City Sports Lounge Mjini Posta, BM Salon Kinondoni, American Nails n Hair Salon,  bila kusahau Nyumbani Lounge mahala patakapofanyika shoo hiyo.