STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, May 8, 2013


HATIMAYE MAHAKAMA YAFUTIA LWAKATARE KESI YA UGAIDI


LWAKATARE

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania leo imetangaza kuyafuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
Taarifa zilizoufikia mtandao huu zinasema kuwa baada ya kufutwa kwa kesi hiyo, ziliripuka shangwe na nderemo kutoka kwa wafuasi wa Chadema waliofika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.
Katika kesi hiyo, Lwakatare alikuwa akiwakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere. (33).

No comments:

Post a Comment