STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, May 8, 2013

Sir Alex Ferguson abwaga manyanya Man Uneted

Kocha wa Man United, Sir Alex Ferguson

LONDON, England
KLABU ya Manchester United imethibitisha leo Jumatano kuwa Kocha Sir Alex Ferguson atastaafu kuinoa timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Ferguson atastaafu Man United akihitimisha zaidi ya robo karne ya kufanya kazi Old Trafford, akisaidia kuipa mataji 20 ya Ligi Kuu ya England hivi  karibuni. 
Fergie, 71 ameiongoza klabu kwa mafanikio ndani na nje ya uwanja, akiingiza klabu hiyo katika soko la hisa la New York Stock Exchange, huku ikikusanya maaamilioni ya mashabiki duniani kote kuanzia mwaka 1986 aliposhika hatamu.
Katika miaka yake 26 ya kuinoa Man United, Ferguson raia wa Scotland ametwaa zaidi ya mataji 30, yakiwamo 13 ya Ligi Kuu ya England – pamoja na huu iliotwaa msimu huu.
Ferguson anatarajia kuaga mashabiki wa klabu hiyo baada ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu msimu huu, ugenini dhidi ya West Bromwich Albion, itakayopigwa Mei 19, taarifa ya klabu ya Manchester United ilisema.
The Sun

No comments:

Post a Comment