MWANADADA mkali wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya nchini, Lady Jaydee ameamua kufuta onyesho lake la miaka 13 tangu awe katika fani hiyo lililokuwa lifanyike Ijumaa kupisha msiba wa Albert Mwangwea 'Ngwair'.
Hatua ya Jide imekuja huku wakali wengine wa muziki huo nchini MwanaFA na Karama Masoud 'Kalapina' ambao nao walikuwa wafanye maonyesho yao Mei 31 jijini dar katika kundi tofauyti.
Jide, ambaye hivi karibuni aliingia kwenye mzozo na kituo cha radio cha Clouds, kiasi cha kufikishwa mahakamani, alinukuliwa akisema kuwa onyesho hilo halitafanyika tena kesho mpaka msiba wa Ngwair utakapomalizika.
Akihojiwa na kipindi cha Super Mix kinachorushwa na kituo cha EA Radio, Jide maarufu kama Komandoo a.k.a Binti Machozi au ukipenda Anaconda, mkongwe alikuwa na wakati mgumu alipoulizwa unamuelezeaje msanii Mangwear.
Jide aliyekuwa mwenye huzuni akijibu huku akilia kuwa, Tanzania imempoteza nyota. Juu ya shoo yake Jide alisema imebidi
aisogeze mbele kidogo mpaka msiba huu upite kwanza ndipo atasema tarehe
rasmi.
Ngwair alifariki jana nchini Afrika Kusini kwa kile kilichoelezwa kuwa kala kitu chenye sumu, taarifa nyingine zikidai alijidunga dawa na kuzimika yeye na rafikie M to the P aliyeripotiwa kulazwa hospitalini akiwa hoi mjini Johannesburg.
No comments:
Post a Comment