STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 30, 2013

Azam Academy yainyuka Ashanti Utd

Azam Academy jana ilicheza na timu ya Ligi kuu ya Ashanti United kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume Ilala na kushinda kwa bao moja bila goli likifungwa na Mshambuliaji wa pembeni toka shinyanga Mange 

Vijana wa Azam Academy wanaonolewa na kocha Vivek Nagul akisaidiwa na Iddi Cheche chini ya meneja Philip Alando walicheza kandanda safi na kuwapoteza kabisa vijana wa Ashani United wanaocheza ligi kuu Tanzania.

Mechi hii ya kirafiki ni ya tatu ndani ya siku nne ambapo siku ya jumatano Azam Academy ilishuka kwenye uwanja wake wa nyumbani na kukwaana na timu ya Transit Camp inayoshiriki ligi daraja la kwanza na kuiangushia kipigo cha 3-1, katika mchezo huo ambao uliacha gumzo kutokana na Azam Academy kutawala mchezo huo wakipiga pasi wanavyotaka.

Baada ya mechi hiyo viongozi wa Transit Camp walikwenda kwa uongozi wa Azam FC na kuwapongeza na kusema kama timu hii ingekuwa inashiriki ligi daraja la kwanza hakika ingeweza kupanda ligi kuu bila matatizo yoyote.

Wachezaji wanaotia fora kwenye kikosi hicho ni Kaijage, Rey, Dismas, Kevin Friday, Mkomola, Mgaya, Mange, Adam Juma, Jamir Brison na Adam Gambo.

Jumamosi Asubuhi licha ya kucheza vizuri na kutawala sehemu kubwa ya mchezo lakini walijikuta wakipokea kipigo cha goli moja bila bao likifungwa na Brian Umony ambaye alitumia vizuri mchezo wa mtego wa counter attack
TIMU ya vijana ya Azam, Azam Academy jana iliinyuka timu ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Ashanti United kwa bao 1-0 katika pambano la kujipima nguvu lililochezwa uwanja wa Karume Ilala.
Vijana hao walipata ushindi huo kupitia bao tamu lililofungwa na mshambulia wao kutoka mkoani Shinyanga aitwaye Mange.
Azam Academy inayonolewa na kocha Vivek Nagul akisaidiwa na Iddi Cheche chini ya umeneja wa Philip Alando waliwafunika kabisa Ashanti kwa soka murua walililoionyesha.
Hiyo ilikuwa mechi ya tatu kwa timu hiyo ya Azam Academy ndani ya siku nne ya awali kuumana na Transit Camp inayocheza Ligi Daraja la Kwanza na kuwakung'uta mabao 3-1 kabla ya kulala bao 1-0 toka kwa kaka zao Azam Fc katika mechi iliyofuata.

No comments:

Post a Comment