|
Beki wa Chuo Kikuu veterani Ernest akimtoka Kudra Omar katika pambano lao la leo |
|
Kudra Omar akichuana na beki wa Chuo Kikuu katika mechi yao ya leo |
|
Beki wa Chuo Kikuu akihamisha mpira langoni mwake huku kipa wake Idd akimshuhudia |
|
Heka heka langoni mwa Chuo Kikuu |
|
Ernest akikokota mpira mbele ya Kudra Omar |
|
Nasafisha! Beki wa Chuo kikuu akihamisha mpira langoni mwake |
|
Onesmo Wazir 'Ticotico' akionyesha kiwango dimbani |
|
Kiungo Shija Katina (8) wa Chuo Kikuu akimtoka Salum Athuman 'Mbududu' wa Golden Bush |
|
Viungo nyota wa zamani nchini Shija Katina (8) na Salum Athuman wakionyeshana kazi |
|
Hupati kitu hapa 'Mbududu' |
|
Shija Katina akimiliki mpira mbele ya Abuu Ntiro |
|
Benchi la Chuo Kikuu likiwa haliamini kama wamelala nyumbani |
|
Beki wa kushoto wa Chuo Kikuu, Ernest (16) akitafuta mbinu za kumtoka Omar Mgonja wa Golden Bush, huku Yahya Issa naye akimpigia mahesabu |
MABAO mawili yaliyotumbukizwa wavuni na nyota wa zamani wa Yanga, Kudra Omar na Abuu Ntiro asubuhi ya leo yalitosha kabisa kuipa ushindi wa mabao 2-1 timu ya Golden Bush Veterani dhidi ya wapinzani wa jadi Chuo Kikuu Veterani katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa Chuo Kikuu.
Golden Bush waliochezesha kikosi tofauti na kile walichokitangaza awali, ilianza kutanguliwa kufungwa bao kupitia kwa Paul mshambuliaji aliyekuwa akiikosesha amani ngome wa Golden Bush iliyokuwa chini ya Salum Swedi 'Kussi', Yahya Issa, Shomari na Omar Mgonja na kipa Aman Simba.
Hata hivyo Golden Bush iliyokuwa ikiongozwa katika safu yake ya ushambuliaji na Kudra Omar, Abuu Ntiro, Onesmo Waziri 'Ticotico' wakiungwanishwa vyema katikati na Godfrey Bonny 'Ndanje' Salum Athuman 'Mbududu'walirudisha bao hilo kupitia kwa Kudra Omar.
Dakika moja kabla ya mapumziko, Golden Bush waliongeza bao la pili lililofungwa na Abuu Ntiro baada ya kutokea pia nikupige klatika lango la Chuo Kikuu lililokuwa chini ya kipa Idd aliyejitahidi kuokoa mabao licha ya kwamba amezoeleka kucheza mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji na kuongeza kasi ya mchezo, na hasa Chuo Kikuu Veterani ambayo ilikuwa ikiunganishwa vyema na Shija Katina aliyeng'ara dimba la kati ambayo ilicharuka kutaka kusawazisha bao lakini kikwazo kikawa ukuta wa wapinzani na hasa kipa Amani.
Mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi aliyelichezesha vyema pambano hilo, Mwenyekiti wa Chuo maarufu kama 'Obama', ilipolia Golden Bush walikuwa wababe mbele ya wapinzani wao waliokuwa uwanja wa nyumbani kwa kuwalaza mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment